Programu bora zaidi kwa ajili ya ku editor video kwenye simu yako kwa watumiaji wa Android na iOS



Programu bora zaidi kwa ku editor video kwenye simu yako hii ni kwa watumiaji wa Android na iOS: Hivi karibuni Instagram imezindua IGTV, sehemu maalum ya video ndefu Pamoja na kuja kwa sehemu hii bado changamoto imekuwa ni jinsi ya kutengeneza hizi video na jinsi ya kuediti video hizo kupitia simu ya mkononi Ramatech tumeliona hilo na leo sisi tuna kuletea program nzuri Programu hizi ni nzuri na ni rahisi sana kutumia na zitakusaidia sana katika ku editi video yako kwa haraka na kwa kutumia simu yako ya mkononi.



  • Antix -video editor GoPro Inc 
Antix-Video editor GoPro ni moja kati ya programu nzuri sana ya ku editi video kupitia simu yako ya mkononi, hii App haina advertising haina sehemu ya kufanya manunuzi inapatikana bure kabisa ku download bonyeza hapa kwa watumiaji wa AndroidDownload hapa
kwa watumiaji wa iOSDownload hapa pia program hii itakusaidia kutuma video harharaka kwenye mitandao ya kijamii kama instagram, Facebook na Youtube



  • KineMaster Pro Video editor
KineMaster ni moja kati ya App za zamani na bora kwaajili ya kuedit video kupitia kwenye simu yako ya Android au iOS. Kama unataka muonekano wa pekee kwenye video zako unazotuma kwenye mitandao ya kijamii basi nakushauri ujaribu programu hii ya KineMaster kwa AndroidDownload hapa
 Kwa iOSDownload hapa



  • PwerDirector Video Editor App: 4K, Slow Mo & More:
Kama simu yako inayo teknolojia ya 4K au hata kama haina na ungependelea kutengeneza video zenye teknolojia hiyo kupitia simu yako ya mkononi basi pakua app hii ya PowerDirector. App hii ni nzuri sana kwa wale wanaopenda video zao kuonekana vizuri na bora zaidi, app hii ni moja kati ya app chache zenye uwezo wa kuweka slow motion kwenye video zako, miongoni mwa mambo mengine mengi Kama unataka utofauti kwenye video zako, pakua sasa app hii lakin app hii ni kwa Android tu Download hapa


  • ActionDirector Video Editor

ActionDirecto video Editor ni app nzuri sana kwa kuedit video kwa haraka, app hii inarakisha sana kazi ya kuediti picha kwa wale watu ambao hawataki kupoteza muda mwingi. App hii ni rahisi kutumia na inaweza kutengeneza video kwaajili ya mitandao mbalimbali ya kijamii hii pia ni kwa Android tuDownload hapa



  • FilmoraGo- Free Video Editor 
 FilmoraGo ni app nyingine nzuri ya kuedit video, tofauti na app nyingine kwenye list hii app ya FilmoraGo itakusaidia kuweka vikorombezo (Effect) kwenye video zako kwa haraka sana. App hii inapatikana kwenye mifumo ya Android na iOS kwa AndroidDownload hapa
Kwa iOSDownload hapa


 Na hizo ndio app nzuri nilizokuandalia leo kwaajili ya kuedit video, kama kuna app nyingine unayo ijua yenye uwezo mzuri wa kuedit video kwenye simu, basi unaweza kutuandikia kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

Maoni