Fahamu zaidi kuhusu Google

Unaitumia Google mara ngapi kwa siku? haya ni mambo ambayo huenda huyajui kuhusu kampuni hiyo:
Haki miliki ya picha Google

Vitu kumi ambavyo huenda hauvijui kuhusu 
Google maisha kabla ya Google? ulifanya nini wakati ulihitaji kutafuta taarifa fulani kwa haraka

Chochote unachokitafuta liwe jina la kitu fulani au jinsi ya kuandika jina fulani au jina la eneo fulani bila shaka ni lazima utafute kwenye Google.

Kwa kukadiria Google hushughulikia karibu mambo 40,000 kwa sekunde moja, hiyo ni sawa na mambo bilioni 3.5 kwa siku.

Google sasa imegeuka kuwa sio eneo tu la kutafuta majina lakini pia sehemu muhimu kwa matangazo na mkusanyaji wa taarifa za watu.

Kila wakati unapofanya kitu fulani, Google inajua kuhusu tabia zetu. Lakini wewe unafahamu mambo yapi kuhusu Google?

Haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kukushangaza.


  • Jina



Kuliandika vibaya jina kati ya marafiki
Google ni nini? kwa kweli neno Google halimaanisha chochote.

Lilitokana na kuandikwa vibaya kwa jina la 'googol'

Kuna madai kadhaa kuhusu labda vile mhandisi au mwanafunzi aliweza kuibuka na jina hilo.

Makosa hayo ya uandishi yalichangia kupatikana nene hilo, na mengine ni historia.


  •  'Backrub'


Awali waalipa Google jina jina 'Backrub'.
Waanzilishi wa Google Larry Page na Sergey Brin awali waliipa Google  jina 'Backrub'.

Haikumaanisha kisugua mgongo lakini ilimaanisha mfumo wa kuorodhesha vitu.

  • Mchezo


Usishangae hamna tatizo lolote na macho yako
Google haihusu tu biashara. Kuna mchezo pia.

Andika jina "askew" kwa Google na ujionee...

  •  Mbuzi
Kuna lishe kwa mbuzi huko Google
Google inasema inaunga mkono mazingira kwa hivyo moja ya njia ni kubadilisha mashine za kufyeka na mbuzi.

Bustani kubwa za makao makuu ya Googleplex huko Mountain View, California, zinahitaji watu wa kuzitunza kila wakati, kwa hivyo kile unachokiona ni karibu mbuzi 200 wanaozunguka huku wakitafuta lishe.

  • Biashara inayokua
Google imekuwa ikinunua kampuni kila wiki tangu mwaka 2010.
Baada ya kuunda kampuni za GMail, Google Maps, Google Drive, Google Chrome...Google imekuwa ikinunua kampuni kila wiki tangu mwaka 2010.

Hautajua lakini kampuni kama Android, Youtube, Waze na AdSense zinamilikiwa na Google na kuna zingine 70.
  • Nembo

Nembo ya kwanza ya Googe au Doodle ilikuwa na nia ya ujumbe wa tarehe 30 Agosti mwaka 1998.

Nembo ya kwanza ya Google au Doodle ilikuwa na nia ya ujumbe wa tarehe 30 Agosti mwaka 1998.

Hilo liliamuliwa wakati Larry na Sergey walikwenda huko Nevada kwa warsha moja iliyofahamika kama (Burning Man Festival) ndipo wakataka watu wafahamu kuwa hawakuwa karibu kuwahudumia.

Tangu wakati huo imekuwa kawaida kwa Google kufanya hivyo kila mara kuashiria siku fulani au watu fulani.

  • Fursa iliyopotezwa lakini si kwa Google


Mgao katika soko
Mwaka 1999 Larry na Sergey walijaribu kuiuza Google kwa dola milioni moja lakini hakuna mtu aliyetaka kuinunua hata licha ya bei kushushwa.

Google kwa sasa ina thamani ya dola bilioni 300. Kuna mtu anajutia sana.

  • Kauli mbiu

'Usiwe muovu' ilikuwa moja ya kauli mbiu ya kwaza ya kampuni hiyo.
'Usiwe muovu' ilikuwa moja ya kauli mbiu ya kwanza ya kampuni hiyo.

Iwapo Kampuni imedumisha hilo au la ni wewe uamue.

  •  Chakula ni muhimu sana

Kuna chakula kila wakati huko Google
Kulingana na jarida la Forbes, mwanzilishi wa Google Sergey Brin aliamua mapema kuwa hakuna ofisi ya Google inaweza kuwa umbali wa mita 60 kutoka mahala kuna chakula.

Kuna uvumi kuwa siku za mwanzo chakula bora kwenye kampuni hiyo kilikuwa ni kitu kilikuwa kinaitwa "Swedish Fish", lakini siku hizi wafanyakazi wa Google, (ambao ni mimi na wewe) wanaweza kupata vyakula vizuri kama kahawa ya kiwango cha juu.

  •  Rafiki mkubwa wa Google.

Wafanyakazi wa Google au wasio wafanyakazi huruhusiwa kupeleka mbwa wao kazini lakini wawe wamefunzwa vizuri wasije wakachafua ofisi.

Kwa habari mbali mbali za teknolojia like page facebook kwa kubofya hii alama 👍

Maoni