Madhara ya simu (Smartphone)

Matatizo ya afya yanayo sababishwa na kutumia simu(SmartPhone) kwa muda mrefu

Simu ni muhimu kwa maisha yetu ya kila siku hasa kwa ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia lakini je,wajua madhala yakiafya yanayo sababishwa na simu (Smartphone)

Pamoja na kuwa simu ina umuhimu kwenye maisha yetu ni vyema kujuwa kwamba chochote kile ambacho utakizidisha sana basi hubadilika na kuwa sumu kwa upande wa simu (Smartphone) nayo huwa hivyo hivyo kwani yapo matatizo mengi ambayo husababishwa na utumiaji wa simu (Smartphone) ulio pitiliza

Sasa kwenye makala hii utaweza kujuwa matatizo matano(5) ya kiafya ambayo hutokea mala nyingi sana na inawezekana ulikuwa hujui nini chanzo cha matatizo hayo ambayo hutokea mara kwa mara kutokana na utumiaji wa simu kwa muda mrefu 

Kama una matatizo haya ambayo mengi yana jirudia rudia mara kwa mara ni vyema kumuona Daktari au kwenda Hospitali au kwenye kituo cha afya kilicho karibu nawe
Baada ya hayo tuangalie madhara yanayo sababishwa na simu (Smartphone)

  • Kuumwa na kichwa na kukosa usingizi

 Kuumwa na kichwa ni moja kati ya dalili inayo ashiria mambo mengi sana kwenye mwili wa Binadamu lakini pia kama umekuwa una umwa na kichwa mara baada ya kumaliza kutumia simu yako au umekuwa ukikosa usingizi mara kwa mara baada ya kutumia simu yako ya mkononi basi inawezekana tatizo hilo lina sababishwa na utumiaji wa simu  yako ya mkononi ulio pitiliza      kama una tatizo hili ni vyema kuwa uwe una pumzika kutumia simu yako kwa muda fulani angalau mara 5 au 10 kila siku,pia hakikisha una achana na tabia ya kutumia simu kabla ya kulala.kumbuka tatizo likizidi ni vyema kumuona Daktari.


  • Maumivu ya mgongo au shingo (Tex tNeck)

Kutokana na utumiaji wa simu (Smartphone) ulio pitiliza watu wengi huweza kupata ugonjwa wa uti wa mgongo amabao kwa kitaalam hutwa Text Neck. Ugonjwa huu hutokea pale mtu anapotumia simu au SmartPhone na kujikunja na wakati mwingine mtu hujikunja hadi kufikia uwiano wa nyuzi 60,hii inaweza kuonekana sio ukunjaji wa shingo wa kiasi kikubwa sana lakini kufanya hivyo kwa muda mrefu huweza kusababisha mgandanizo kwenye eneo linalo jikunja na hivyo kufanya mtu kupata maumivu ya mara kwa mara anapo nyoosha sehemu hiyo ya shingo.
Kuepukana na tatizo hili unashauliwa kutumia simu kwa muda wa kawaida na pia hakikisha unatumia simu kwa usawa sio kwa kujikunja sana pia tatizo hilo likizidi usiache kumuona Daktari.

  • Kuona kwa shida au kuwasha kwa macho
Kuona kwa shida inaweza ikawa ni chanzo cha magonjwa mengine hatari ya macho yako , lakini kama umekuwa ukiona kwa shida mara baada ya kutumia simu yako pengine hiyo ni dalili ya matatizo yanayo sababishwa na matumizi ya Smartphone yaliyo pitiliza mara nyingi hii hutokea pale unapotumia simu yako kwa mwanga hafifu sana au kwa mwanga mkali sana. Ni vyema kumuona Daktari maalum wa macho pale unaposikia dalili yoyote ya tofauti ya macho yako.

  • Vidole vya mikono kufa ganzi mara kwa mara
Kama umekuwa na tatizo la kufa ganzi kwenye mikono mara kwa mara ni vyema uwende kumuona Daktari,lakini pia kama umekuwa na tabia ya kushika simu yako mkononi kwa muda mrefu huwenda hii ikawa ni moja ya sababu inayo sababisha vidole vyako vya mikono kufa ganzi mara kwa mara. Hakikisha unaiweka simu yako mfukoni au mezani pale unapokuwa huitumii.

  • Ugonjwa wa kupenda  Smartphone
Moja kati ya tatizo ambalo watu hudhani kuwa ni tatizo ni kupenda Smartphone sana ugonjwa huu umethibitishwa na madaktari na ni moja kati ya tatizo kubwa sana miongoni mwa watumiaji wa simu hizi za kisasa maarufu kama Smartphone.kujuwa zaidi kuhusu tatizo hili unaweza kusoma hapa➡Madhala ya Smartphone kwa leo tutaishia apa unaweka uka like facebook page kwa habari mbali mbali kwa kubofya tu hii alama apa➡👍 

Maoni