Udukuzi wa akaunti milioni 50 za Facebook wapata ufumbuzi:

Akaunti milioni 50 za Facebook zimeingiliwa Facebook wapata ufumbuzi:
                           Haki miliki ya pichaREUTERS



Facebook imesema zaidi ya watu milioni 50 akaunti zao zimeingiliwa na wengine zilijaribiwa kuingiliwa na wavamizi.

Kampuni hiyo imesema kuwa wavamizi walichunguza katika sehemu za miundo ya akaunti kwa watumiaji.

Tatizo hili liligundulika siku ya Jumanne, na Facebook wameshatoa taarifa polisi.

Watumiaji ambao wameathirika na uvamizi huo wameambiwa wataruhusiwa kuingia kwa mara ya nyingine tena kuanzia wiki ijayo.

Kampuni imetoa taarifa kuwa tatizo litakuwa limetatuliwa Makamu wa Rais wa Facebook Guy Rosen amesema tatizo limekwisha, huku akaunti nyingine milioni 40 zimewekwa kwenye uangalizi maalum.

Tangu kuibuka kwa tatizo hilo Facebook bei ya ushirikiano imeshuka kwa asilimia 3 hasa siku ya Ijumaa na huku zaidi ya watumiaji bilioni mbili wamekuwa wanatumia mtandao huo.

Wakizungumza na Waandishi wa habari viongozi wa Facebook wamesema imewatahadharisha watumiaji wawe makini na wavamizi wa mtandaoni pamoja kwamba wamesuluhisha shida hiyo.

Hii ikimaanisha kuwa makampuni mengine makubwa kama AirBnB na Tinder yapo katika hatari ya kuwamiwa na wavamizi.


Nani ameathirika na hilo?


Kampuni imewashauri watumiaji waingie kupitia akaunti zile zile na nywila bila kubadirisha.

"Tangu tumeanza uchunguzi huu bado hatujagundua kama akaunti zilitumiwa vibaya au taarifa yoyote mbaya iliingia. Na hatujui kitu kilichopo nyuma ya pazia kwa wavamizi hawa".

Aliongeza kuwa faragha za watu na usalama wa watu ni muhimu sana na tunaomba msamaha kwa kilichotokea.

Kampuni imetoa taarifa kuwa mwazilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg na Mkuu wa Utendaji Sheryl Sandberg ni miongoni mwa watu milioni 50 walioathirika na uvamizi huu.

Facebook imeeleza kuwa faragha za watu kuonekana hasa wasifu wa watu si vizuri kiusalama. Kitu ambacho kilipelekea taarifa zilionekana kwa marafiki,na marafiki wengine na kwa jamii yote.

Wavamiza walivumbua mbinu mpya zilizofanya kuchukua baadhi ya taarifa za Facebook , lilipelekewa kuingiliwa kwa akaunti nyingine. Alisema Mr Rosen

"Kuingia katika mfumo huo unaofanana na kuwafanya watumiaji kuingia kwenye akaunti zao bila kuingiza Nywila iliwasaidia wavamizi kuingia kwenye akaunti za watu, ambapo wanatumia njia mpya ya kuingilia'.


Hii ina maanisha nini kwa facebook?
Wavamizi wamekuja wakati ambapo Kampuni ya Facebook wanawashawishi wanasheria kutoka Marekani katika namna ya kulinda matumizi ya taarifa za wengine.

Mwazilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kwenye mkutano na Wanahabari kuwa Kampuni imejizatiti katika usalama wa watumiaji ingawa waliingiwa wakati wako katika hali ya kujilinda vizuri.

Makamu wa Rais Bwana Jeff Pollard na Mkuu wa uchambuzi wamesema Facebook inapokea taarifa nyingi za faragha ni lazima ikubwe na sikendo kama hizi.

"Wavamizi waliingia kwenye faragha za watu siku za karibuni imekuwa kawaida kwa Facebook kuingiliwa mara kwa mara kutokana na kutunza vitu vya watu. Alisema.

Kitu kikubwa wavamizi walingilia usalama wa Zaidi ya watumiaji milioni 10.

"Hii inaonyesha Facebook inahitaji kuzuia faragha za watu na kuweka kipaumbele kwa watumiaji.

Alipoulizwa na BBC alishindwa kufunguka kama uchunguzi utajikita kwenye kuelezea kukosekanika kwa usalama.

Pia walishindwa kuonyesha kama watakuwa tayari kumuwajibisha yeyote kwenye Kampuni kama atakuwa amehusika na uvamizi wa taarifa.
 Usisahau ku subscribe kwenye hii blog kwa habari mbali mbali pia tembelea Facebook kwa kubofya hii alama 👍

Maoni